Mawaziri wa Serikali ya awamu ya Tatu, Basil Mramba na Daniel Yona wameanza kutekeleza rasmi adhabu ya kufanya usafi katika hopitali ya Sinza Palestina, kama sehemu ya masharti ya kifungo cha nje.

Mawaziri hao wamewasili katika eneo la hospitali hiyo leo na kukabidhiwa vifaa vya usafi.

Mkurugunzi wa Huduma za Jamii mkoa wa Dar es Salaam,Deogratias Shirima alieleza kuwa Mawaziri hao wamepata nafasi ya kuona eneo la kufanyia kazi. Alisema kuwa wote kwa pamoja wamekubali kuanza kufanya kazi kama walivyoelekezwa kwa saa nne.

Leo, saa nne zilikamilika wakati wakiwa wanaoneshwa maeneo yao ikiwa ni pamoja na mtaro unaopitisha maji machafu.

Magufuli aipa mahakama Mabilioni, serikali yasema zitasaidia hukumu ya wakwepa kodi
Wachina waadhimisha mwaka mpya wa Nyani kwa mtindo wa pekee