Mawaziri wapya wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar waliopishwa leo Machi 4, 2021, wamesema wamejipanga kumsaidia Rais Dkt. Hussein Mwinyi ili kukidhi matarajio makubwa waliyonayo Wazanzibari katika kupata maendeleo.

Mwaziri hao wwameeleza hayo leo wakizungumza na vyombo vya habari ambapo Waziri wa Nchi ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais, Saada Mkuya Salum amesema atahakikisha utekelezaji wa  sera ya uchumi  unafanyika kuambatana na  usimamizi mzuri wa mazingira yaliopo.

Aidha, amesema atahakikisha sera na sheria zote zitakazotungwa na kutekelezwa nchini zinazingatia masuala yote mtambuka.

Kwa upande wake Waziri wa Afya ,Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto Nassor Ahmeid Mazrui amesema, “ Chini ya usimamizi wa Rais, tumejipanga kutoa huduma bora kwa wananchi.”

Naye Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, Omar Said Shaaban amesema atafanya kila juhudi kuhakikisha Zanzibar inarejea katika hadhi yake ya kuwa kitovu cha Biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.

Shaaban ameongeza kuwa ili kufanikisha azma ya Uchumi wa Buluu, atahakikisha Zanzibar inanufaika na malighafi zote za bahari.

Kujifukiza Muhimbili Tsh. 5000
Azam FC wafichua siri ya ushindi wa Kagera