Mawaziri wawili wa zamani wa Zimbabwe wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya mali za umma na kujihusisha na rushwa.

Samuel Undenge ambaye alikua waziri wa nishati anatuhumiwa kutumia dola elfu kumi na mbili kwa kampuni ambayo hewa.

Aidha, kwa upande wa wake, Walter Mzembi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Robert Mugabe aliyeondolewa madarakani mwezi Novemba, anatuhumiwa kuchangia baadhi ya mali za televisheni ya Taifa katika Kanisa moja nchini humo bila ya idhini ya serikali.

Hata hivyo, Rais mpya, Emmerson Mnangagwa ameapa kupambana na rushwa iliyodumu kwa muda mrefu wakati wote wa utawala wa Robert Mugabe.

Muisrael akamatwa kwa kuuza viungo vya Binadamu
Waliojiuzulu ubunge wateuliwa na CCM