Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amewataja mawaziri watano wenye mahudhurio hafifu Bungeni na kwenye kamati za Bunge.

Amewataja mawaziri hao hii leo bungeni jijini Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu kwa waziri mkuu, Kassim Majaliwa.

Aidha, mawaziri hao ni pamoja na Dkt. Agustine Mahiga (Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa) mwenye asilimia 5; January Makamba (Muungano na Mazingira) asilimia 37; Profesa Palamagamba Kabudi (Katiba na Sheria) asilimia 38; William Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) asilimia 41 na Luhaga Mpina (uvuvi na mifugo) asilimia 45.

 

Breaking News: Mbunge wa jimbo la Temeke (CUF) ajiuzulu
Wabunge wanne waliohama Chadema waapishwa Bungeni

Comments

comments