Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Marcio Maximo ni miongoni mwa makocha wanaotajwa kuomba nafasi ya kuinoa kikosi cha klabu ya Young Africans.

Maximo alipata mafanikio makubwa akiwa kocha wa Stars kati ya mwaka 2007 na 2010, na alirejea nchini mwaka 2014 kujiunga na Young Africans akiletwa nchini na aliyekuwa Mwenyekiti wa kwa wakati huo Yusufu Manji

Hata hivyo alishindwa kufikia malengo na kujikuta anaonyeshwa mlango kutokea miezi sita baadaye.

Kocha huyo raia wa Brazil anaamini kutofanikiwa kwake mara ya kwanza ilikuwa bahati mbaya na akipata nafasi nyingine atafanya vizuri.

Maximo ni miongoni mwa makocha zaidi ya sitini ambao wametuma wasifi (CV) zao Young Africans.

Zipo taarifa kuwa hata kocha wa sasa wa Taifa Stars Etienne Ndayiragije, naye amejitosa kuomba nafasi ya kukinoa kikosi cha Young Africans kuanzia msimu ujao.

Uongozi wa Young Africans umeahidi kuwa watakamilisha mchakato na kumtangaza kocha mkuu mapema kabla ya timu kuingia kambini katikati ya mwezi huu.

Makonda akabidhi ofisi Dar es Salaam
Fedha za FIFA kunufaisha mikoa Tanzania Bara, Zanzibar