Beki wa Southampton Maya Yoshida amekubali kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu ambao utaendelea kumuweka klabuni hapo hadi mwaka 2020.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 29, raia wa Japan ameshaitumikia Southampton katika michezo 138 tangu alipotua nchini England mwaka 2012 akitokea club VVV-Venlo ya Uholanzi.

Makamu mwenyekiti wa klabu ya Southampton Les Reed amesema wamekamilisha mpango wa kumsainisha mkatana mpya beki huyo, na wamejihisi faraja kuendelea kuwa na Yoshida, ambaye ameonyesha uwajibikaji tangu walipomsajili miaka miaka mitano iliyopita.

Yoshida amesema “Ninajihisi furaha kuendelea kuwepo hapa kwa miaka mjingine mitano, naamini nitapambana kikamilifu ili kuiwezesha Southampton kufikia malengo yake”,

Aliongeza: “Najihisi nipo nyumbani.”

Video: Tukamateni Chadema wote mtuweke rumande- BAVICHA
Ndoa Ya Man Utd Na Zlatan Yafungwa Upya