Kocha Mganda wa Simba SC, Jackson Mayanja amefunguka nakusema kwa mfumo wanaotumia Yanga SC anaweza kuwafunga katika mechi itakayochezwa jumamosi katika uwanja wa taifa.

Mayanja aliuambia mtandao huu  kuwa Simba in aweza kushinda hata mabao 3-0 kutokana na mfumo wanaotumia Yanga wa 4-3-3

” Nimeisoma mifumo anayoitumia Pluijm Yanga na nimejaribu kutafuta mbinu za kutegua mbinu zake anazotumia”amesema Mayanja

Pluijm kwenye michezo mingi amekuwa akitumia mfumo wa 4-3-3, ambao ni mfumo unaohitaji washambuliaji watatu wenye kuweza kucheza kitimu, lazima wawe na uwezo binafsi utakaowawezesha kuibeba timu inapozidiwa,”amesema kocha huyo wa zamani wa Kagera Sugar.

Isaac Mwangi: Nitajiuzulu Kwa Muda
Ronaldo Ashangaza Kwenye Mkutano Na Waandishi Wa Habari