Bondia Floyd Mayweather amewashangaza wadau wa soka baada ya kuweka wazi nia yake ya kutaka kuinunua klabu ya Newcastle United inayoshiriki ligi kuu nchini Uingereza na kumsajili rafiki yake Ronaldo ambaye kwa sasa anachezea Real Madrid.

Mmiliki wa Klabu ya Newcastle Mike Ashley, Alikaribia kuiuza timu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana lakini zoezi hilo lilishindikana.

“Inabidi uamini kama nikiwekeza Newcastle nitakuwa nikirudi kusherekea mara kwa mara’’ amesema Mayweather wakati akizungumza na Daily Star.

Mayweather ambaye amekiri kuvutiwa na mji wa Newcastle kutokana na starehe zilizopo na jinsi ambavyo wananchi wa mji huo wanajua kusherekea amesema mara zote amekuwa akifikiria fursa ya kufungua biashara mpya na michezo kwani ni kitu ambacho anakipenda.

“Napenda michezo, lakini nawekeza kwa kutumia kichwa sio moyo wangu. Ukiwekeza kwa kutumia mapenzi ya moyo wako ni njia rahisi ya kupoteza pesa, lakini kama kuna mtu anaweza leta mpango wa biashara na watu wangu wakautizama na kuupitisha nina weza kuwekeza. Soka inaweza kuwa sio mchezo wangu lakini nina mtandao kila sehemu. Ronaldo ni mtu wangu wa mda mrefu, hivyo naweza kumpata akamalizia kucheza mpira akiwa Newcastle’’ amesema mwanamasumbwi huyo anaye sifika kwa kuwa na majigambo na matanuzi ya pesa.

Newcastle United kwa sasa inakamata nafasi ya 13 kwenye ligi kuu nchini Uingereza ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza michezo 30.

Deschamps asema Paul Pogba 'hana raha' Old Trafford.
Mchungaji awalambisha viatu waumini wake