Siku chache baada ya kumalizika kwa pambano kubwa la masumbwi lilolompa ushindi Mfilipino, Manny Pacquiao dhidi ya Timothy Brandley, bondia aliyestaafu bila kupigwa, Floyd Mayweather amepinga matokeo hayo.

Pambano hilo lilifanyika Wikendi iliyopita katika ukumbi wa MGM, Arena Garden Grande, Las Vegas nchini Marekani.

Kwa mujibu wa ESPN, Mayweather anaamini kuwa hakukua na mshindi katika pambano hilo na kwamba ilipaswa kuwa ‘sare’ bali kelele za mashabiki wa Pacquiao ndizo zilizowachanganya majaji wakajikuta wanampa ushindi Pacquiao.

Pacquiao vs Bradley second Fight Result

Inaelezwa kuwa Mayweather alimpigia simu Brandley na kumueleza kuwa ana uhakika hakushindwa pambano hilo na kwamba kama haamini inabidi aende akaangalie tena mkanda wa pambano hilo akiwa amezima sauti.

Mayweather ambaye alimshinda Pacquiao kwenye pambano lao lilipewa hadhi ya ‘pambano la karne’, alimwambia Brandley kuwa ameimarika zaidi na kumtaka kuendelea na mchezo huo.

Hata hivyo, maelezo ya Mayweather yamepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki wa mchezo huo, kwani Mbali na kwamba majaji wote watatu walimpa ushindi Pacquiao, Brandley aliangushwa mara mbili kwa ngumi za Mfilipino huyo.

Kadhalika, Brandley hakuonesha kupinga maamuzi ya majaji hao akieleza kuwa alifanya kwa kiwango chache cha mwisho lakini Pacquiao alikuwa bondia bora zaidi usiku huo.

 

Hilo lilikuwa pambano la tatu kati yao, ambapo mara ya kwanza walipigana mwaka 2012 na Brandley aliibuka na ushindi uliopingwa na wengi akiwemo Pacquiao aliyedai anaamini alishinda. Mwaka 2014, Pacquiao alimshinda Brandley na kulipa kisasi.

Cristian Brocchi Meneja Mpya AC Milan
West Ham Utd Wadhamiria Kumrejesha Carrick Jijini London