Bingwa wa zamani wa masumbwi, Floyd Mayweather Jr. amepanga kuanza mafunzo ya mateke kwa lengo la kujiunga na mapambano ya UFC/MMA.

Akizungumza TMZ, bingwa wa UFC, Tyron Woodley amesema kuwa alikutana na Mayweather na kuzungumza naye kuhusu mpango huo katikati ya mwezi uliopita.

“Floyd Mayweather anapenda kuingia kwenye mchezo wa kupigana ngumi na mateke. Kwahiyo aliyechaguliwa kumfunza mbinu hizo ni nani? [ni mimi pekee],” Woodley aliiambia TMZ.

Alieleza kuwa wanaandaa mipango na kwamba wanaweza kuanza mafunzo muda wowote.

Akizungumzia muda atakaotumia kumfunza mbinu za kupigana ngumi na mateke, kukabana na mieleka inayohusika kwenye UFC, alisema kuwa Mayweather ambaye amestaafu akiwa ameshinda mapambano yote 50 bila kupoteza au kutoa sare anahitaji muda mfupi.

“Kwa mateke, anahitaji wiki mbili au tatu. Kwa mbinu za mieleka itafanana kidogo na masumbwi, kwa sababu mchezo wa masumbwi una kona nyingi, kuchezesha kichwa na miguu inahusia zaidi,” alisema.

Alitoa mfano wa wapinanaji wengi wa UFC ambao hawana mbinu za mieleka ambao wanajiita wapiganaji hodari wakiwa wamesimama.

Mamlaka ya Hali ya Hewa yatoa tahadhari na angalizo kwa wananchi
Black Panther yazidi kupaa, yapiga $bilioni 1

Comments

comments