Imeelezwa kuwa Kobe Bryant na binti yake wa miaka 13, Gianna Bryant wamezikwa tayari na kwamba mazishi ya wawili hao yamefanyika kwa siri sana katika eneo la Pacific View Memorial Park huko Corona Del Mar, California, Ijumaa, Februari 7 mwaka huu.

Kwa mujibu wa mtandao wa E-News, Mazishi ya nyota huyo wa zamani wa NBA yalihudhuriwa na mkewe, Vanessa Bryant, na watoto wake wengine watatu walioshiriki ambao ni Natalia(17), Bianka (3) na Capri, miezi 7, Vanessa na familia walitaka kufanya tukio hilo kwa siri.

Vanessa alithibitisha kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa siku maalumu ya kumuaga Kobe Bryant na binti yake Gianna ni tarehe 24/2/2020 tarehe ambayo inaendana na namba ya jezi aliyoitumia wakati akiicheza Los Angeles Lakers.

“Sherehe hiyo ya kumuaga ingekuwa ngumu sana kwa kila mtu kwani bado ni ngumu kwao kuamini kuwa wamepoteza watu wao wawili ambao wanawapenda sana.”ameandika Vanessa kupitia ukurasa wake wa instagram.

Hata hivyo tarehe ya tukio la kutoa heshima za mwisho kwa halaiki litabaki hivyo hivyo licha ya maziko kuwa yamefanyika tayari.

FebruarI 24″ ni tarehe maalumu, kwani ndio nambari ya Kobe aliyoitumia akicheza kwenye safari ya maisha yake tangu msimu wa 2006-07.

 

TANESCO yalipa fidia Bil. 1.99 kwa wakazi wa Same
NEC: Hatujatangaza ratiba ya uchaguzi mkuu

Comments

comments