Uamuzi uliofanywa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wa kuhamishia fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao FC kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma utakaopigwa Mei 28 mwaka huu mekuja mara baada ya kuelezwa kuwa Uwanja wa taifa utafungwa kwa ajiri ya matengenezo.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka Dodoma, kimesema kuwa siri kubwa ya fainali hiyo kuchezwa mkoani humo ni kuhusiana na kuandaa mazingira ya uchaguzi mkuu wa TFF ambao unatarajiwa kufanyika mapema mwaka huu.

Chanzo hicho kimesema kuwa tayari kuna mipango ya chini kwa chini ambayo inafanywa na ngazi za juu za uongozi ndani ya TFF YA kumpigia kampeni Mwenyekiti wa Chama cha Soka mkoani humo,  Mlamu Ng’ambi ambaye anatakiwa kuendelea kuwa kiongozi ndani ya Shirikisho hilo.

“Hii fainali ina mambo mengi lakini kwa taarifa yako wamealikwa baadhi ya wajumbe wanaounga mkono upande flani kuhudhuria fainali zitakazofanyika hapa Dodoma ili wajipange kuhusu uchaguzi,” kimesema chanzo hicho.

Kwa mjibu wa Gazeti la michezo la BINGWA, mtoa habari huyo alisema kuwa mtoa habari huyo amesema kuwa katika fainali hizo wajumbe wote walioalikwa katika fainali hiyo watalipiwa posho ya usafiri wa ndani, posho ya kutosha na huduma muhimu wakapokuwa Dodoma.

Kwa mujibu wa kanuni, Simba ndio wenyeji wa mchezo huo kwa sababu ndio walitangulia kutinga fainali hizo kwa kuwafunga Azam bao 1-0 kwenye mchezo wa nusu fainali kabla ya Mbao walioichapa Yanga bao 1-0 kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali, katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Video: Majaliwa aagiza huduma za afya zisifungwe wakati wa zoezi la usafi
Ngassa atamba kuitandika Yanga