Baada ya kuachiliwa huru kwa mwanafunzi wa Kimarekani aliyekuwa amefungwa gerezani nchini Korea ya Kaskazini, Otto Warmbier na muda mfupi baadaye kufariki dunia, familia yake imekataa mwili wake kufanyiwa uchunguzi ili kujua hasa kilisababisha kupoteza maisha.

Mwanafunzi huyo alifariki dunia jumatatu Ohio nchini Marekani mara baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani nchini Korea ya Kaskazini alikokuwa akishikiliwa kwa takribani miezi 15.

Otto Warmbier alihukumiwa kwenda jela miaka 15 na kufanya kazi ngumu Machi 2016 baada  ya kushtakiwa kwa kosa la kuiba bango lililokuwa likieneza Propaganda katika hoteli moja nchini Korea Kaskazini.

Madktari katika hospitali Cincinnati jimbo la Ohio aliyokuwa akitibiwa mwanafunzi huyo wa kimarekani mara baada ya kuachiliwa huru 13, June mwaka huu wamesema kuwa kijana huyo alikuwa akisumbuliwa na tatizo la kupoteza fahamu baada ya ubongo wake kuathirika.

Korea ya Kaskazini imedai kuwa kukosa kwake fahamu kulitokana na kutiliwa Sumu katika chakula na dawa za usingizi lakini madaktari wa Marekani na familia yake wamekana taarifa hiyo.

Video: Haponi mtu, Siri ya jaji mwingine kujiuzulu
Magazeti ya Tanzania leo Juni 21, 2017