Wananchi visiwani Zanzibar wamekumbwa na hofu kutokana na kuwepo ripoti za baadhi ya watu kushambuliwa na watu wasiojulikana wanaoficha sura zao wanaojiita ‘Mazombi’.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar

Watu hao wanaodaiwa kuvaa soksi za kufunika sura zao, wanadaiwa kujeruhi watu kwa kutumia silaha za moto na silaha za jadi hususan katika maeneo ya Mjini Magharibi, Unguja.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limesema kuwa halijapata taarifa kuhusu matukio hayo ya ‘Mazombi’ lakini wananchi wameendelea kuelezea uwepo wa matukio hayo.

Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omari ameeleza kuwa suala hilo linawapa utata kwa kuwa hakuna mwananchi yoyote aliyewahi kuripoti kuhusu matukio hayo na wao wameendelea kusikia kama tetesi.

“Kama kuna suala linatusumbua ni hili la Mazombi. Wananchi mtusaidie kufikisha ujumbe huu, yeyote atakayedhuriwa na hao watu aje kutoa taarifa au apige simu namba za usalama akiwa eneo la tukio ili iwe rahisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu hao, hatuwezi kushughulikia kesi bila kuwa na ushahidi,” Kamisna Omari anakaririwa.

Mazombi hao wanadaiwa kuwa ndio waliotekeleza tukio la kuchoma kituo cha redio cha Hits Fm cha Migombani, Unguja mwaka jana.

Baadhi ya wananchi wameeleza kuwa waliwahi kuwashuhudia mazombi hao wakifanya tukio wakiwa wamevalia mavasi yanayofunika nyuso zao, huku wananchi wengine wakiwaonesha waandishi wa habari maganda ya risasi wanayodai waliyaokota kwenye eneo la tukio la Mazombi hao.

Angalizo: Picha ya habari ni mchoro wa maana halisi ya mazombi wa kusadikika 

Wajumbe Hawa wa ZEC wapinga marudio ya uchaguzi Zanzibar
Polisi wafariki kwenye Msafara wa Rais Magufuli