Vyama vikuu vya siasa nchini Ujerumani vya Social Democrats, SPD, Kijani na Free Democrats, FDP vimesema huenda vikakamilisha majadiliamo ya ya kuunda serikali ya muungano wiki hii.

Ingawa havijatoa tamko rasmi kuhusiana na majadiliano hayo yaliyofanyika siku ya Jumatatu, vyama hivyo vimesema vinataka kusuluhisha kwanza tofauti zao kwa faragha.

Vyama hivyo bado vinatofautiana katika masuala kadhaa ambayo ni pamoja na sera zinazohusiana na kodi pamoja na mabadiliko ya tabianchi.

Katibu mkuu wa SPD Lars Klingbeil amesema baada ya mazungumzo ya siku kadhaa zilizopita wanaamini kwamba wataweza kuafikiana iwapo watashughulikia tofauti hizo.

Kwa mujibu wa Idhaa ya Kiswahili (DW) Uchunguzi wa maoni wa hivi karibuni umeonyesha asilimia 51 ya waJerumani wanaunga mkono muungano wa serikali wa SPD, FDP na Kijani, huku wengi wakionyesha kutotaka chama cha Christian Democrats cha kansela Angela Merkel kuunganishwa kwenye serikali, ingawa kilishinda nafasi ya pili kwenye uchaguzi.

Iwapo makubaliano yatafikiwa siku ya Ijumaa, chama cha Kijani kimesema kitahitaji kufanya kongamano dogo la chama litakaloidhinisha uwepo wao ndani ya serikali. Wamesema watafanya mkutano huo siku ya Jumapili ili kutoa maamuzi haraka.

Southgate kusaini mkataba mpya England
COSOTA yapokea Utaratibu wa kusambaza filamu kwenye mabasi