Siku moja baada ya kuthibitishwa kuwa meneja mpya wa klabu ya Watford, Walter Mazzarri anajiandaa kutuma ofa kwenye klabu ya Palermo ya nchini kwao Italia, kwa lengo la kumsajili kiungo Oscar Hiljemark.

Kiungo huyo kutoka nchini Sweden amekua chaguo la kwanza la Mazzarri kufuatia upungufu alioukuta klabuni hapo wa wachezaji wanaaocheza nafasi ya katikati ya uwanja.

Mazzarri, anaamini kama atafanikiwa kumsajili Hiljemark mwenye umri wa miaka 23, atapa ahuweni ya kukisuka vyema kikosi cha Watford ambacho msimu uliopita kilikua kikinolewa na meneja kutoka nchini Hispania, Enrique “Quique” Sánchez Flores.

Main ImageMeneja mpya wa klabu ya Watford Walter Mazzarri (Kushoto), Enrique “Quique” Sánchez Flores (Kulia) aliyeachana na klabu hiyo ya England juma lililopita.

Hata hivyo Hiljemark, anawania na klabu za AC Milan na SSC Napoli zote za nchini Italia, hivyo huenda Mazzarri akapata wakati mgumu wa kumuondoa katika ligi ya Sirie A.

Tayari rais wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini ameshatangaza kumuweka sokoni Hiljemark, na amesisitiza atafurahi kukamilisha biashara hiyo kabla ya fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016 (Euro 2016) ambazo zitaanza rasmi Juni 10 huko nchini Ufaransa.

Video: Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Sekouture kuanza kutoa huduma kwa watoto njiti
Magwiji Wa London Wapigana Vikumbo