Vitambulisho vya wajasiriamali kufanyiwa maboresho na ukomo wa matumizi ya kitambulisho hicho utakuwa ni mwaka mmoja mara tu baada ya mhusika atakapo lipia na si kuisha muda kulingana na kalenda ya mwaka.

Hayo yamesemwana naibu Waziri Tamisemi, Dk Festo Dugange leo Juni 22, 2021 bungeni Jijini Dodoma ambapo amebainisha kuwa lengo la mabadiliko hayo ni kupunguza usumbufu.

Naibu waziri Dugange, akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Hawa Mchafu aliyeihoji Serikali ina mpango gani wa kurasimisha vitambulisho vya wajasiriamali.

Amesema vitambulisho hivyo vilirasimishwa kutumiwa na wajasiriamali wenye mitaji na mauzo ghafi yasiyozidi Sh4 milioni.

“Kuanzia mwaka 2021 vitambulisho vya wajasiriamali wadogo vimefanyiwa maboresho kadhaa ikiwemo kuwekwa picha na jina la mjasiriamali mdogo na inamuwezesha kutambuliwa,” amesema Dugange.

Bunge lavunja rekodi bajeti mwaka wa fedha 2021/22
Waliodhaniwa kubeba msiba wasababisha ajali