Huenda klabu ya Mbao FC yenye maskani yake jijini Mwanza ikaondoka mikononi mwa wanachama, na kuingia kwenye umiliki wa muwekezaji ama mmiliki mpya.

Mipango ya klabu hiyo kuondoka kwenye umiliki wa wanachama, inatajwa kusababishwa na hali ngumu ya kiuchumi inayoendelea kuikabili klabu hiyo ambayo inashiriki ligi kuu kwa msimu wanne mfululizo.

Uongozi wa timu hiyo umeiweka Sokoni timu hiyo na tayari watu mbali mbali wameanza kujitokea kuonyesha nia yakutaka kuinunua .

Mwenyekiti ya Klabu hiyo Solly Njashi alinukuliwa akisema kuna moja ya Wilaya za mkoa wa Mwanza zimeweka dau mezani, lakini bado hawajafikia muafaka.

Mbao FC inashika nafasi ya 19 kwenye msimamo ya ligi kuu ya Tanzania bara msimu huu wa 2019/20,  na ligi itakaporejea itakuwa na mtihani wa kujipapatua ili iondoke kwenye janga la kushuka daraja.

Katika hatua nyingine aliyekuwa Katibu mkuu wa klabu hiyo Daniel Naila alitangaza kujiuzulu katika nafasi yake juma lililopita, huku sababu ikitanjwa kuwa ni mwenendo mbaya wa timu.

Mbao FC pia iko kwenye hatua za mwisho za kumtangaza Kocha mkuu mpya, baada ya kumuondoa kocha Hemed Morocco mwezi mmoja uliopita.

Waziri Mkuu kuongoza mamia kumuenzi Mengi
Corona: Saudi Arabia marufuku kutoka nje usiku kujikinga