Kikosi cha Mbao FC kimeshindwa kuwika katika uwanja wake wa nyumbani wa CCM Kirumba jijini Mwanza, kwa kukubali matokeo ya sare ya bila kufungana katika mchezo wa ligi kuu ya soka Tanznaia bara uliowakutanisha na Lipuli FC ya Iringa.

Matokeo hayo yanaendelea kuiweka pabaya Mbao FC kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara, kwani mpaka sasa imeshajikusanyia alama 20 baada ya kucheza michezo 23 na kuendelea kukamata nafasi ya 14.

Mbao FC ipo juu ya timu za Njombe Mji FC inayoshika nafasi ya 16 kwa kufikisha alama 18 zilizopatikana katika michezo 22, huku Majimaji FC wakiburuza mkia kwa kuwa na alama 16 walizozipata ndani ya michezo 22 waliyocheza.

Kwa upande wa Lipuli FC imefikisha alama 28 baada ya kucheza michezo 23 na kuendelea kukamata nafasi ya saba katika msimamo wa ligi kuu, ikiwa juu ya Mbeya City na Ruvu Shooting ya Pwani zenye pointi 25 kila moja baada ya kucheza michezo 22.

JPM atengua uteuzi wa Mkurugenzi
Singida Utd yatulizwa Namfua stadium

Comments

comments