Mshambulaiji wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG Kylian Mbappe na beki wa pembeni wa majogoo wa jiji Liverpool Trent Alexander-Arnold wametajwa kwenye orodha ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora mwenye umri mdogo (Kopa Trophy).

Waratibu wa tuzo ya Ballon d’Or wametangaza orodha ya wachezaji 10 watakaowania Kopa Trophy, ambayo inawahusisha wachezaji walio chini ya umri wa miaka 21.

Wengine waliotajwa kwenye orodha hiyo ni mlinda mlango wa klabu ya  AC Milan  Gianluigi Donnarumma, Patrick Cutrone (AC Milan) pamoja na Justin Kluivert (AS Roma).

Orodha hiyo pia imemjumuisha kinda la kibrazil lenye umri wa miaka 17 kutoka klabu ya Santons, Rodrygo Silva de Goes.

Rodrygo anatajwa kuwa kwenye mipango ya kujiunga na mabingwa wa soka barani Ulaya Real Madrid, wakati wa dirisha dogo mwezi Januari mwaka 2019.

Mshindi wa tuzo ya Kopa Trophy atatangazwa kwenye hafla za Ballon d’Or Disember 03 mjini Paris.

Orodha ya wanaowania Kopa Trophy.

  1. Houssem Aouar (Lyon)
  2. Trent Alexander-Arnold (Liverpool)
  3. Patrick Cutrone (AC Milan)
  4. Ritsu Doan (Groningen)
  5. Gianluigi Donnarumma (AC Milan)
  6. Amadou Haidara (RB Salzburg)
  7. Justin Kluivert (AS Roma)
  8. Kylian Mbappe (Paris Saint-Germain)
  9. Christian Pulisic (Borussia Dortmund)
  10. Rodrygo (Santos)
Video: Chukua tahadhari katika bichi hizi, ni hatari kwa maisha yako
Video: Mtoto wa Suge aonesha video anayodai ni Tupac ‘yuko hai’ Malaysia

Comments

comments