Wakati mtikisiko wa uhamisho wa Neymar kuelekea Paris Saint-Germain (PSG) ukiendelea kuwachanganya wadau wa Soka duniani, ripoti za kinda mpachika magoli Kylian Mbappe kuachana na klabu ya Monaco zinahusishwa na mpango wa kuliziba pengo lililoachwa kwenye ngome ya ‘MSN’.

Kwa mujibu wa jarida la L’Equipe, ingawa Mbappe ananyemelewa na vilabu vikubwa ikiwa ni pamoja na Real Madrid, Barca ambao wana kiu ya kupata mbadala wa Neymar ndio wanaonesha nia zaidi kumsajili.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyeng’ara na kikosi cha Monaco katika Ligi ya Mabingwa msimu uliopita alitarajiwa kuongeza mkataba kwa dau la £160m, lakini mambo yamekuwa ndivyo sivyo.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa moyo wa Mbappe uko zaidi katika klabu ya Real Madrid lakini biashara inaweza kumvuta Barcelona ambayo ina mtaji wa £198m kutoka kwa uhamisho wa Neymar. Kinda huyo ana mtihani wa kung’ara katikati ya Luis Suarez na Karim.

Mbali na Mbappe, wachezaji wengine wanaotajwa zaidi kunyemelewa na Barcelona kuziba pengo la Neymar ni pamoja na Ousmane Dembele (Borussia Dortmund), Paulo Dybala (Juventus, Philippe Coutinho (Liverpool) na Antoine Griezmann (Atletico Madrid).

Sethi anyimwa kutibiwa nje ya nchi
Alshabaab washambulia basi la abiria na kuua, polisi wawavaa