Kadi nyekundu ya mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbarak Yusufu imefutwa, na sasa yupo huru kucheza mchezo wa mwisho dhidi ya Azam FC utakaofanyika Mei 20, 2017.

Uamuzi huo umefikiwa katika kikao kilichokaa juzi na kupitia taarifa mbalimbali za michezo iliyochezwa, ambapo kamati ilijiridhisha kuwa mwamuzi alimpa kimakosa kadi nyekundu mshambuliaji huyo.

Wakati Mbaraka akiruhusiwa kucheza mchezo ujao, mwamuzi aliyechezesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar, Ngole Mwangole ameondoshwa kwenye orodha ya waamuzi wa ligi kuu.

Ngole Mwangole ambaye alipewa taji la mwamuzi bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Mbaraka Yusuph katika mchezo ulioishia kwa Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 2- 1.

Edinson Cavani Aula, Afunika Ligi ya Ufaransa
Toto waahidi kulitoa tone la mwisho Kuikaba Yanga Wasishuke