Mshambuliaji mahiri wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbaraka Yusuph Abeid leo alienda TFF kuchukua nakala ya mkataba wake.

Pamoja na kwamba, sisi kama Azam tulikuwa na nakala halisi ambayo iliwasilishwa TFF kwenye usajili ulioisha. Lakini tulimwambia Mbaraka akachukue nakala yake TFF.

Cha kustaajabisha ni kwamba, leo hii TFF imempatia mbaraka nakala mbili za mkataba ambazo moja inaonyesha mkataba uliosainiwa ni wa mwaka mmoja na mwingine ambao umefojiwa ukionyesha ni wa miaka 3.

Mkataba mmoja umesainiwa tarehe 20 June 2016 na mwingine ukiwa ni wa tarehe 10 Agosti 2016.

Mkataba wa tarehe 20 June, umesainiwa ukionyesha mwaka mmoja na ule wa 10 Agosti ni 2016 ni miaka mitatu. Ukiacha tofauti ya miezi mitatu ya kusainiwa mikataba hii, lakini hata kiwango cha usajili ni tofauti mno.

Hata hivyo, mkataba wa miaka mitatu, umesainiwa bila kuwa na saini ya mchezaji, wala muhuri wa klabu ya Kagera Sugar n ahata jina la Mchezaji kwenye sehemu ya kusaini halijaandikwa.

Tutaiweka hadharani mikataba hii kwa idhini ya mchezaji ili familia ya mpira ione mikataba yote miwili na kisha tarataibu nyingine zifuate.

Kuna uhuni mwingi ambao unafanywa kwenye baadhi ya mambo kwenye mpira wetu, hasa masuala ya mikataba ya wachezaji, Sisi Azam tunataka kulimaliza tatizo hili. Na kwa hili tutatumia wanasheria wetu kuwafikisha mahakamani wote walioshiriki kufoji mkataba wa Mbaraka ili kujenga precedent nzuri huko mbele

Nitumie nafasi hii kuwaomba Kagera Sugar, ama kukanusha au kuthibitisha juu ya mikataba hii ili hatua stahiki ziweze kufuatwa.

Suala la kufoji mikataba ya wachezaji ni uhuni ambao haupaswi kuchwa kuendelea kwenye mpira.

#TimuBoraBidhaaBora
#azamfcdiehardfans

Magazeti ya Tanzania leo Juni 21, 2017
Marehemu alipiwa mahari Msumbiji