Waziri wa Mawasiliano, Uchukuzi na Ujenzi, Prof. Makame Mbarawa leo amezindua bodi mpya ya Shirika la Reli Tanzania (TRL) na kuitaka kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wafanyakazi wote wa shirika hilo.

Amsema hayo alipokuwa katika uzinduzi huo makao makuu ya shirika hilo jijini Dar es salaam, na kuisisitiza bodi hiyo kuwa waadilifu na wazalendo, ameongeza kuwa kama mtu akishindwa kusimamia uadilifu basi hana nafasi ya kufanya kazi katika shirika hilo.

Aidha, Mbarawa amesema TRL inajukumu kubwa la kukabiliana na soko la ushindani ambalo linashikiliwa na malori makubwa ya usafirishaji, amesema kuwa kazi kubwa ni kutoa huduma nzuri ambazo zitawashawishi wateja kutumia usafiri huo ambapo itasaidia kujipatia masoko mengi zaidi.

Walioteuli katika bodi hiyo ya TRL ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa chuo mstaafu cha DIT, Prof. John Wajanga Kandoro ambaye ndiye mwenyekiti wa bodi hiyo, wengine ni Linford Mboma alikuwa mwenyekiti TRC, Miriam Mwanilwa kutoka Ofisi ya Rais bodi ya mishahara, Martha Maeda kutoka TIB, Mhandisi Charles Mvungi kutoka TIB,na Mashaka Mabuyu ambaye ametoka WFB.

Wachezaji Wa Arsenal Wahofiwa Kuchoka
Video: 'Hatutaki mgao wa umeme' - Waziri Muhongo