Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa ameitaka Bodi mpya ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuhakikisha wanatokomea na kudhibiti ongezeko la wizi mtandaoni.

Ameyasema hayo alipokuwa anazindua Bodi hiyo na kueleza kuwa watanzania wameibiwa kwa muda mrefu kupitia njia ya ujumbe mfupi (SMS) na kushawishiwa kutoa fedha kwa udanganyifu na hivyo kuitaka Bodi hiyo kutofumbia macho changamoto hiyo.

“Changamoto ya wizi mtandaoni inagusa watanzania wengi, mkiwa na jukumu la kudhibiti mna wajibu wa kuwalinda wananchi wote,hivyo nnahitaji mdhibiti changamoto hiyo ya wizi”amesema Mbarawa.

Aidha, Mbarawa ameitaka Bodi hiyo ya TCRA kusimamia kwa ukaribu sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika kudhibiti ubora wa mawasiliano ikiwa ni teknolojia inayokua kwa kasi kubwa.

Hata hivyo mbali na kutoa maagizo hayo ,Mbarawa pia ameitaka bodi hiyo  kuendelea kudhibiti meseji za uchochezi zinazotumwa na wananchi kwa kukosa maadili.

Tendwa: Vyama vingi vilitokana na vuguvugu la wananchi
Watanzania kuadhimisha miaka 55 ya uhuru