Vijana watatu wa kiume wanashikiliwa na vyombo vya usalama kwa kosa la kumbaka msichana huku wakionesha tukio hilo moja kwa moja kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, Jumatano wiki hii.

Martin Milan na Rayford Smith wenye umri wa miaka 19 pamoja na Antun Hester mwenye umri wa miaka 18 walikamatwa katika eneo la Memphis, Tennessee nchini Marekani. Walifanya tukio hilo kwa msichana mwenye umri wa miaka 17.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa polisi, msichana huyo alikuwa amekubaliana na Milan kukutana nyumbani kwao kama wapenzi, lakini Milan alikuja na rafiki zake wengine wawili.

Msichana huyo aliwakatalia rafiki zake kuingia chumbani kwake na akaingia na Milan peke yake, lakini baadaye wote walimvamia na kumbaka kwa zamu huku wakionesha kwenye mtandao wa kijamii.

Baada ya tukio hilo, msichana huyo alikimbia kwenye choo cha bibi yake na kuwapigia simu polisi ambao walifika na kuwakamata watuhumiwa wote.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, watuhumiwa watafikishwa mahakamani Ijumaa ya wiki ijayo.

 

 

Thamani ya Facebook yaporomoka kwa $58 bilioni, kashfa yaiponza
Horn Vs Crawford lahamishiwa kwa Mayweather Vs Pacquiao

Comments

comments