Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema Polisi wanamshikilia Charles Majura (35) ambaye ni Fundi Simu, kwa kosa la kimtandao kwa kusambaza taarifa za uzushi kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ni Mgonjwa.

Kamanda Kingai amesema kumekuwa na tabia ya baadhi wa Watu pindi wanapotumiwa taarifa za uzushi nao wanasambaza bila kujua kuwa ni kosa kisheria na kusema wanaendelea kuwafuatilia wote wenye tabia hiyo na wakikamatwa watafikishwa Mahakamani.

Kingai ametoa kauli hiyo Mkoani Pwani baada ya kikao kilichojumuisha Makamanda wa Polisi wa Mikoa minne ya Pwani, Morogoro, Tanga na Kinondoni.

Miradi 281 ya maji kuzinduliwa
Kenya yapiga marufuku mikutano ya kisiasa