Mwenyekiti wa Chama C cha NCCR Mageuzi James Mbatia ameipongeza Serikali kwa kulitambua janga la corona na kuchukua hatua za kuhamasisha na kuelimisha wananchi kujinga na janga hilo.
 
Amesema hayo wakati wa mkutano wake na Waandishi wa habari mkoani Dar es salaam.

Ambapo ameshauri kufanyika kwa tathmini ya corona nchini, itakayosaidia kuwekwa vipaumbele na usimamizi utakaosaidia  kukabiliana na maambukizi zaidi.
 
Aidha, Mbatia amesema kuwa takwimu za  ugonjwa wa corona Barani Afrika zinaonesha katika wimbi la tatu la ugonjwa huo kuna ongezeko la asilimia 43 ya maambukizi ikilinganishwa na wimbi la kwanza na la pili, hivyo tahadhari zaidi inahitajika.

Waziri Mkuu ajiuzulu kwa kushindwa kunda Serikali
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Julai 17, 2021