Mgombea Ubunge wa jimbo la Vunjo kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia, ameupinga uamuzi uliotolewa na kamati ya maadili jimbo hilo wa kumfungia kwa siku saba kutofanya kampeni kuanzia leo Jumamosi tarehe 17 hadi 23 oktoba 2020.

Mkuu wa idara ya Uenazi na Mahusiano wa NCCR-Mageuzi, Edward Simbeye amesema,”uamuzi huo ni ubatili, kikao kilichofanyika ni batili na tunaendelea na kampeni kama kawaida.”

Simbeye aliyeko jimboni kwa mbatia amesema, vipeperushi vinavyozungumzwa vinaelezea mambo aliyoyafanya Mbatia kwa kipindi cha miaka mitano (2015-2020)

Amesema, kwa mujibu wa maadili ya uchaguzi kipengele cha 5:4 kinazungumzia, kama kuna maadili yamekiukwa, “kiwasilishe kwa msimamizi kwa njia ya maandishi, lakini CCM haijafanya hivyo,tuliomba kupewa hayo malalamiko yao kwa maandishi, hatukupewa.”

Simbeye amesema, baada ya Mbatia ambaye pia ni mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi kupewa malalamiko hayo, “aliyajibu lakini cha kushangaza, katika kikao cha jana utetezi wake aliouwasilisha kwa maandishi, haukusomwa, sasa unawezaje kuamua bila kusikiliza utetezi wa anayelalamikiwa.”

Pia, amesema, kikao kilichokaa jana, kilihusisha majimbo mawili jambo ambalo ni kinyume na taratibu za uchaguzi “yaani mgombea wetu, amehukumiwa na vikao viwili vya majimbo badala ya kimoja. Ndiyo maana tunasema ni batili na sisi tutaendelea na kampeni kama kawaida kesho”.

Zanzibar na Serikali ya muungano kutatua changamoto tano
Baraza la Mambo ya Nje UE hofu ya kuenea kwa Covid 19