Wagonga Nyundo wa Jiji la Mbeya ‘Mbeya City’ leo Ijumaa (Machi 10) watashuka katika Dimba na Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya kuendelea na Mshike Mshike wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Ruvu Shooting.

Mbeya City wanarejea nyumbani jijini Mbeya baada ya kuibanjua Kagera Sugar mjini Bukoba mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa Hatua ya 16 Bora Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’ na kutinga Robo Fainali.

Kocha Msaidizi wa Mbeya City ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Tiger FC, Anthony Noliega Mwamlima amesema wamekamilisha maandalizi ya mchezo huo na wana matarajio makubwa ya kuendelea kufanya vizuri.

“Maandalizi yetu yamekamilika na wachezaji wako tayari kwa mapambano ili kuibuka na ushindi na kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri katika msimamo,” amesema Mwamlima

Mbeya City inaelekea katika mchezo wa leo ikiwa imeshajikusanyia alama 27 zinazoiweka nafasi ya 10 katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku Ruvu Shooting ikiendelea kuburuza mkia kwa kuwa na alama 17.

Meridianbet 'watimba kibabe' na Odds kubwa
Sixtus Mapunda ndani, Nyamsenda nje Ukuu wa Wilaya