Orodha ya  wachezaji ambao  walikuwa kwenye kikosi cha Mbeya City fc msimu uliopita  na mikataba yao kufikia tamati baada ya kumalizika kwa  ligi  kuu ya vodacom Tanzania bara  mei 22  tayari  imetolewa  ikiwataja nyota saba kutokuwepo tena  kikosini  msimu ujao.

Muda mfupi uliopita, Katibu Mkuu wa City Emmanuel Kimbe amesema kuwa, wachezaji saba wanaotajwa kwenye orodha  hii ni wazi mikataba yao imemalizika na klabu haitafanya tena  mazungumzo yoyote  na tayari wamesha taarifiwa  juu ya hilo.

“Mikataba yao imemalizika, tumekwisha wataarifu kuwa hatutakuwa na mazungumzo mapya, hili soka  kutoka timu moja kwenda nyingine ni jambo la kawaida  hivyo tunawatakia kila la heri kwenye maisha mapya ya soka watakayo kutana nayo” alisema.

Kwenye orodha hiyo  yupo mlinda mlango Haningtony Kalyesubula, walinzi ni  Yusuph Abdalah Sisalo,Deo Julius,Hamad Kibopile,Yohana Morris, Richard Peter Chundu na mshambualiaji Temmi Felix.

Katika hatua nyingine Kimbe amesema kuwa klabu bado inafanya mazungumzo na baadhi ya nyota ambao  mikataba yao imemalizika lakini bado wanayo nafasi ya kuendelea kukitumikia  kikosi cha City kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha Kinnah Phiri, huku pia mazungumzo ya wachezaji wengine ambao bado wana mikataba lakini hawapati nafasi ya kucheza yakiendelea ili kuona ni jinsi gani wanaweza kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.

Orodha ya wachezaji hao  pamoja na wale wanaoendelea kuitumikia klabu itatolewa hapo baadae.

Zijue Silaha za Kulinda Maahusiano Yako
Video: Rais Magufuli Apata Pongezi Kutoka Jukwaa Huru la Wazalendo Tanzania