Mshambuliaji wa Azam FC, Didier Kavumbagu ameanza mazungumzo na Mbeya City na huenda hii leo inaweza kumtangaza rasmi kuwa mchezaji wao.

Taarifa za ndani ya Mbeya City zinasema kwa asilimia kubwa, Kavumbagu raia wa Burundi na Mbeya City wamemalizana.

Ofisa Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba amesema hawana tatizo kama Mbeya City na Azam FC wamemalizana.

“Hatjui kama wanazungumza na kama wanazungumza basi hakuna tatizo kwa kuwa mkataba wetu na Kavumbagu umebaki siku chache tu,” alisema.

Lakini mtu mwingine kutoka ndani ya Mbeya City amesema, klabu hiyo inatarajia kumtangaza Kavumbagu rasmi kesho.

Warabu Kuchezesha Young Africans Vs Mouloudia Olympique Bejaia
Serengeti Boys Kambini Juni 13 Kuanza Kujifua Kombe La Mataifa Afrika