Serikali Mkoani Mbeya, inayoshika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa madini Tanzania baada ya mkoa wa Geita, inaendelea kuweka mazingira nafuu kwa wawekezaji kwenye sekta ya madini ili kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera wakati akifanya mahojiano na TBC na kusema Rais Samia amefuta leseni kubwa, ili kuwapa fursa wawekezaji wadogo hasa kwenye misitu ya Mbiwe na Itumbi ili kukuza sekta ya madini.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.

Amesema, asilimia 10 ya mikopo inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya Vijana, Wanawake na wenye ulemavu kwa mkoa wa Mbeya, kutakuwa na kipaumbele kwa wale wanaojihusisha na uchimbaji wa madini.

Juni 2022, Kituo cha Uwekezaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini kilifungua milango ya utoaji wa vibali kwa wachimbaji wadogo katika Sekta ya Nishati na Madini, watakaotenga maeneo makubwa ya uwekezaji kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na uchenjuaji wa madini.

Matumizi fedha mbichi: DC awashukia watendaji
Migogoro ya ardhi: Shaka akemea watumishi wala rushwa