Vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Young Africans kesho Jumatano (Januari 19), itacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbuni FC mjini Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Young Africans imeweka kambi mjini Arusha kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania, utakaopigwa mwishoni mwa juma hili Uwanja wa Ushirika mjini Moshi-Kilimanjaro.

Benchi la ufundi la Young Africans limependekeza mchezo huo wa kirafiki, ili kuwa sehemu ya maandalizi ya kikosi chao, kuelekea mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, ili kuendelea kufanya vyema katika Mshike Mshike wa Ligi Kuu msimu huu 2021/22.

Mbuni FC itakayocheza na Young Africans kesho Jumatano, inashiriki Ligi daraja la kwanza (FL), ikiongoza msimamo wa Kundi B kwa kufikisha alama 17.

Martial akanusha tuhuma Man Utd
Ziara ya Rais Mwinyi UAE imezaa matunda