Wakati mchakato wa kuwania Uspika wa Bunge la 11 ukiendelea, imeelezwa kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), imebaini mpango wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa kutumia nguvu ya Lowassa ndani ya CCM kumpata spika wanayemtaka.

Kwa mujibu wa taarifa zilizochapishwa kwenye gezeti ya Raia Mwema, mmoja kati ya makada wa CCM aliyewania nafasi ya kugombea urais kwenye kura za maoni alithibitisha kuwepo njama hizo.

Alisema kuwa Ukawa wanataka kutumia nguvu ya Lowassa kupitia wabunge wa chama hicho wanaomuunga mkono, ili kupitisha jina la Spika wanayemtaka atakayelinda maslahi yao.

“Lengo la Ukawa ni kutumia nguvu ya Lowassa ndani ya CCM ili chama kipeleke majina matatu yote wapambe wake ili mmoja achaguliwe kuwa Spika,” anakaririwa Kada huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

“Wanataka kulitumia bunge la 11 kwa maslahi ya Lowassa, kwamba wahakikishe Spika atakayekuja analiendesha Bunge wanavyotaka wao na kukwamisha kabisa mwenendo wa Serikali ya awamu ya Tano,” aliongeza.

Hata hivyo, Kada huyo alieleza kuwa tayari chama chao kimeshaandaa mkakati wa kuzuia mbinu hiyo.

“Wala usishangae kama Ukawa hawatapeleka Dodoma mgombea uspika. Lakini tumewashtukia majina ya watu wao hayatapenya CCM.”

 

 

 

 

Gabon, Sudan Zakwama Kombe La Dunia 2018
Ban Ki-Moon Ampongeza Rais Magufuli