Taasisi ya Tanzania Health Summit imeandaa mbio za nusu Marathon ambazo zinatarajia kufanyika tarehe 26 April 2017  katika barabara ya Kaole na kumalizikia Coco beach Masaki Jijini Dar es salaam .

Aidha, mbio hizo zinalengo la kusaidia upimaji wa afya na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza magonjwa yasiyoambukiza.

Hayo yamesemwa mapema hii leo na Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo, Rebecca John alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuhamasisha jamii kushiriki katika mbio hizo.

“Kamati ya maandalizi ya ya mbio za Heart Marathon inapenda kuwa taarifu wadau wote wa Sekta ya Afya hapa nchini na jamii kwa ujumla juu ya mbio za Heart Marathon na upimaji wa afya ili kuungana na Serikali katika juhudi za kupunguza magonjwa yasiyoambukiza” amesema Rebecca.

Aidha, amesema kuwa kwa mwaka huu mbio hizo zitashirikisha washiriki zaidi ya elfu mbili kutoka rika mbalimbali wakiwemo vijana, watoto, wazee, makundi ya watu wenye ulemavu na watu wenye magonjwa yasiyoambukiza.

Hata hivyo, Rebecca ameongeza kuwa washiriki watapata nafasi ya kupima afya magonjwa mbalimbali kama vile shinikizo la damu ,wingi wa sukari katika damu, kiasi cha mafuta mwilini, uchunguzi wa uvimbe katika matiti na kupata ushauri wa wataalam kuhusiana na vyakula bora, magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Kwa upande wake Rais wa Tanzania Health Summit, Dkt. Omary Chillo amesema kuwa washiriki watatakiwa kutoa kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kununua  flana pamoja na kifaa maalum cha kuhesabia muda wakati wa kukimbia ila maji ya kutosha yatatolewa bure kwa ajili ya wakimbiaji.

 

Video: Waziri Ummy atoa ufafanuzi kuhusu ajira za madaktari
Rais Kenyatta Atoa Onyo Kuhusu Uchaguzi wa Kenya