Aliyekuwa Mbunge wa Shinyanga Mjini na Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP), Stephen Masele amechukua fomu ya kugombea Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo January 10,2022 katika Ofisi ndogo za CCM Lumumba Dar es salaam.

Hapo jana Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilitangaza kuanza mchakato wa kumsaka mrithi wa nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai ambaye alijiuzulu tarehe 6 Januari mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari, Visiwani Zanzibar, Katibu wa NEC- Itikadi Uenezi CCM, Shaka Hamidu Shaka amesema mchakato huo utaanza kuanzia tarehe 10 hadi 30 Januari mwaka huu.

Hatua hiyo imekuja baada ya Job Ndugai kuandika barua kwa hiari yake ya kuachia nafasi hiyo na kuwasilisha kwa Katibu Mkuu wa CCM jijini Dodoma.

Dkt. Tulia achukua fomu za U-Spika
Mbowe arejeshwa Mahakamani baada ya mwaka Mpya