Mbivu na mbichi ya wateule watatu watakaopitishwa kwa kupigiwa kura na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya Spika wa Bunge, itajulikana leo.

Mchakato huo unaendelea pia kwenye Chama cha ADC ambacho ni kati ya vyama vya upinzani chenye mgombea, Maimuna Kassim, aliyejitokeza kuchukua fomu ya kuwania kiti hicho kilichoachwa wazi.

Wateule ndani ya CCM watajulikana baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya chama hicho kupitisha majina matatu yatakayopelekwa kwa hatua zaidi.

Kamati hiyo iliyokutana jana na leo ndiyo inayokamilisha mchakato huo baada ya kupokea majina yaliyopitiwa na sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho.

Sekretarieti hiyo ilikutana Januari 17, mwaka huu, kujadili na kuishauri Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa wagombea waliojitokeza kuomba kiti hicho.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa awali Januari 9, mwaka huu na Katibu Idara ya Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Shaka Hamdu Shaka, urejeshaji fomu ulikamilika Januari 15, mwaka huu.

Neema yawashukia wachimbaji wadogo
Simba SC kuifuata Mtibwa Sugar kesho