Mahakama nchini Kenya imeongeza muda wa zuio la tume ya mishahara nchini humo juu ya wabunge kujiongezea kiasi cha posho wanayopewa ili kuboresha hali zao za maisha.

Wabunge nchini kenya walipitisha azimio la kujiongezea posho ili kuboresha hali za maisha yao katika upande wa makazi, kwa kulipana posho maalum kwaajili ya nyumba ambayo ni kiasi cha shillingi za kitanzania milioni 5.5 kwa kila mbunge ambayo itakuwa ikitolewa kila mwezi.

Baada ya azimio hilo, tume ya mishahara nchini humo mnamo mwezi oktoba mwaka jana iliamua kufungua kesi ili kupinga ongezeko la posho hiyo ya nyumba kwa wabunge, kwa kueleza kuwa malipo hayo ya fedha kwa wabunge ni matumizi mabaya ya fedha za umma.

kwamujibu wa taarifa ambayo imetolewa imeeleza kuwa mahakama imeamua kusogeza muda wa kusikiliza shauri hilo hadi julai 24 mwaka huu.

Endapo azimio hilo litapitishwa, wabunge 416 wa bunge tukufu la Kenya watapokea kiasi hicho cha malipo kila mwenzi.

Shambulio la aibu lampandisha kizimbani
Serikali yataifisha mali zenye thamani ya Tsh. bilioni 93.16