Mshambuliaji mpya wa Azam FC Mkon­gomani, Idris Mbombo wamemtumia Salamu mfungaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara John Bocco kwa kusema atafunga sana msimu wa 2021/22, ambao umepangwa kuanza mwishoni mwa mwezi huu Septemba.

Mbombo ametoa tambo hizo baada ya kufunga bao moja katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Horseed ya Somalia, kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho, uliochezwa Azam Complex Chamazi Jumamosi (Septamba 11).

Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Azam FC akitokea El Gouna inayoshiriki Ligi Kuu nchini Misri, aliifunga bao la pili dakika ya 73 ya mchezo huo dhidi ya Horseed FC.

Mbombo amesema: “Kwangu kama mchezaji ni jambo la kushukuru Mungu ku­weza kufunga bao ambalo limeisaidia timu yangu kupata ushindi muhimu siku ya Jumamosi dhidi ya Horseed ya Somalia.”

“Licha ya kufunga bao hilo lakini binafsi naona bado nina kazi kubwa ya kufanya, ili kurejea katika kiwango changu, hii ni kwa sababu kwa muda mrefu nilikuwa benchi kule El Gouna, hivyo nitapambana mazoezini ili kufunga mabao mengi zaidi kwa kila nafasi nita­kayoaminiwa na kocha.”

Mabao mengine ya Azam FC katika mchezo huo yalifungwa na Ayoub Lyanga na Lusajo Mwaikenda.

Young Africans yakanusha taarifa za Kocha Nabi
Rivers United kujipima kwa Enyimba FC