Mchezaji bora barani Afrika mwaka 2016 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) atatangazwa leo, katika hafla maalum zitakazofanyika nchini Nigeria.

Wanaoshindania tuzo hiyo ni kiungo wa kati wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, winga wa Algeria Riyad Mahrez na winga wa Senegal Sadio Mané.

Mohamed Salah wa Misri na Islam Slimani wa Algeria walikuwa kwenye orodha ya wachezaji watano bora lakini waliondolewa kutokana na kura zao kutofikia idadi ya kuridhisha.

Kwa upande wa tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika, kwa wachezaji wa ligi za mataifa ya Afrika inawaniwa na mlinda mlango Uganda Denis Onyango anashindana na mshambuliaji wa Zimbabwe Khama Billiat na kiungo wa kati wa Zambia Rainford Kalaba .

Mshindi atatangazwa mjini Abuja, Nigeria saa nne na nusu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

 

Orodha kamili ambayo itaonekana kwenye luninga (Screen) za ukumbini.

WANAOSHINDANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA

Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Borussia Dortmund)

Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

Sadio Mané (Senegal & Liverpool)

 

WANAOSHINDANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA (Ligi za Afrika)

Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns)

Rainford Kalaba (Zambia & TP Mazembe)

 

Kwa upande wa burudani utaongozwa na msanii mkubwa kutoka nchini Tanzania Diamond Platnumz anayetamba na kibao chake cha Salome.

Jerry Muro Ajutia Makosa, Aomba Msamaha Wa Rais
Nyota Ya Juuko Murushid Yang'aa, Kukipiga AFCON 2017