Mwanafamilia wa WCB, Mbosso amesema kuwa ana ndoto ya kumfanyia kitu kikubwa Bosi wake, Diamond Platinumz ili kukumbuka fadhira alizomfanyia na kubadili maisha yake.

Akitoa maoni yake kuhusu uamuzi wa Harmonize kuchora tattoo yenye picha ya Diamond, alisema yeye anaweza kufanya kitu kingine tofauti miaka kadhaa ijayo.

Akifunguka kupitia Radio One, Mbosso amesema kuwa kwa sasa haoni kitu ambacho anaweza kumfanyia Diamond zaidi ya kumuombea kutokana na uhalisia wa kipato chake, lakini miaka kadhaa ijayo anaota kumnunulia jumba la kifahari, gari la kifahari au uwanja wa gharama.

“Siwezi kumlipa fadhira Diamond kwa kile alichonifanyia, nitampa nini mimi zaidi ya kumuombea dua kwa Mwenyezi Mungu, lakini kwa miaka minne mitano ijayo huwezi jua naweza kumfanyia,” alisema Mbosso.

“Huwezi jua, mimi naweza nisimchore Diamond kama alivyofanya Harmonize, lakini Mungu akijalia miaka ijayo huwezi kujua… naweza nikamjengea nyumba moja kubwa ya kifahari, au kumnunulia gari zuri la kifahari au hata uwanja mzuri, yaani kitu chochote kikubwa cha kumuonesha shukurani,” Mbosso ameongeza.

Mwanafamilia huyo wa zamani wa Yamoto Band ambaye amesema kuwa alikutana na Diamond kwa mara ya kwanza mwaka 2012, amekuwa msanii aliyetoa nyimbo zilizofanikiwa sana akiwa WCB hususan kuanzia nusu ya mwaka jana.

Mwaka 2016, Hamornize alichora mkononi tattoo yenye sura ya Diamond aliyemtambulisha kwenye mkondo mkuu wa muziki nchini, na hivi sasa ni msanii anayefahamika nje ya Afrika na kufanya ‘collabo’ na wasanii wakubwa ndani na nje ya Afrika.

Solskjaer ammulika Sanchez, adai yajayo yanafurahisha
Video: UVCCM, UDSM yafafanua faida za Ndege Mpya