Mahakama Kuu ya Tanzania kitengo cha ardhi imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) kuhusu kurejea katika jengo iliyokuwa ofisi ya Tanzania Daima na ukumbi wa Bilcanas.

Akitoa hukumu hiyo leo Oktoba 18, 2016 Jaji mfawidhi wa mahakama hiyo, Sivangilwa Mwangezi amesema kuwa taratibu zote zilifuatwa kuondoa vitu vya Mbowe Hotels Ltd katika jengo hilo hivyo katika hukumu hiyo hakuna aliyevunjiwa hazi yake ya msingi kutokana na kufuatwa kwa sheria dhidi ya madai ya NHC kwa Mbowe Hotels.

Wakili wa NHC, Aliko Mwamnenge amesema kutokana na hukumu hiyo Mbowe Hotels wanadaiwa sh. Bil. 1.7 na NHC, hivyo vitu haviwezi kurudishwa mpaka alipe deni lake kwa NHC.

Kwa upande wa Wakili wa Mbowe Hotels, John Mallya mara baada ya uamuzi huo wa Mahakama Kuu amesema wamepokea hukumu na kuomba nakala ili kuweza kuifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kuamua kama wanaweza kukata rufaa.

  • Shirika la Nyumba la Taifa NHC September 1 2016 lilivamia na kuondoa vifaa katika chumba cha habari cha gazeti la Tanzania Daima linalomilikiwa na Mbowe Hotels chini ya Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Ni ‘Jihad’ Nangwanda Sijaona Kesho
Je, wajua Mwalimu Nyerere ndiye chanzo China kujulikana Kimataifa? Haya hapa mambo 18 mazito