Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake leo, Jumatatu, Agosti 23, 2021 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa hati ya dharura.

Washtakiwa hao wamelazimika kufikishwa mahakamani hapo, kufuatia mwendesha mkuu wa mshtaka (DPP) kukubali kuhamishwa kwa kesi hiyo kutoka kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kupelekwa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Kesi hiyo inalazimika kuhamishwa kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwenda Mahakama kuu, kutokana na kuhusishwa makosa ya Uhujumu uchumi na Ugaidi ambayo hayawezi kusikilizwa katika mahakama ya ngazi ya chini.

Mara ya mwisho Mbowe na washtakiwa wenzake walifikishwa katika Mahakama ya Hakumu Mkazi Kisutu juma lililopita na kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 27 mwaka huu.

Gomes awaweka kitako wachezaji wake
Hoja 18 kujadiliwa kamati ya pamoja SMT na SMZ