Hatimaye Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amezungumzia hatua ya aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Edward Lowassa kurejea katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mbowe ameeleza kuwa walimkaribisha Lowassa kwenye chama hicho mwaka 2015 kama ilivyo jukumu la chama cha siasa kuongeza idadi ya wanachama na kwamba katika kutekeleza jukumu hilo, vyama huvutia watu wa aina mbalimbali.

“Wapo watu wema, wapo watu wasio wema, wapo wanaotaka madaraka, wapo wanaoendeshwa na wito wa kuwatumikia watu na justice (haki), sasa kila mmoja katika uelewa wake anaelewa anataka nini. Kwahiyo, japo meza hii tupo Chadema watupu inawezekana kuna baadhi yetu ambao tuna ajenda za ziada ambazo hatuzijui, sasa kila mmoja anakuwa na malengo japo tunagemea kuwa na melengo yanayofanana,” amesema Mbowe.

Ameeleza kuwa kazi wanayoifanya ni ngumu na inahitaji uvumilivu kwani wapo walioanza mapema wakaishia njiani, wapo waliowakuta wameshaanza safari nao wakaishia njiani na kuna walioingia karibuni ambao nao waliachia njiani.

“Katika kuihubiri haki na kulaani yasiyo na mashiko, katika kulifanya hili unahitajika wajibu na kazi hii ni ngumu,” ameeleza.

Aidha, Mbowe ambaye ameweka wazi kuwa taarifa za Lowassa kurejea CCM zilimsikitisha, amemtaka mwanasiasa huyo kusema ukweli akiwa ndani ya chama hicho ili iwe msaada.

“Nilisikitika, nikisema nafurahi nitakuwa muongo, lakini kwenda katika chama kingine cha siasa basi akasema ukweli na itusaidie kwamba chama chake kipya kisiendelee kuwatesa, na mjadala huu naufungia hapa,” alisema Mbowe.

Lowassa alitangaza kurejea CCM wakati ambapo Mbowe alikuwa bado mahabusu kufuatia kufutiwa dhamana yake pamoja na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko.

Akizungumza kuhusu Chadema aliyoihama, Lowassa alisema anawashukuru viongozi na wanachama wa chama hicho ambacho kilimpa nafasi ya kugombea urais mwaka 2015 akiungwa mkono na vyama vilivyounda Ukawa.

Korea Kaskazini waeleza kifuatacho baada ya Trump na Kim kushindwana

“Kwa Chadema, nawashukuru viongozi wa Chadema na nawashukuru wanachama wa Chadema…msiniwekee maneno mdomoni,” alisema Lowassa baada ya kupokelewa Monduli, jimbo alilolitumikia kwa miaka 20 kama mbunge wa CCM.

Magaidi waua watu 49 wakifanya ibada msikitini

Malawi: Joyce Banda ajiengua mbio za urais
Serikali yashauriwa kuandaa mpango mkakati wa kunusuru Ziwa Manyara