Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameionya Tume ya Uchaguzi (NEC) kuhusu ukiukwaji, upuuziaji na uzalilishaji kwa wapinzania kwenye uchaguzi mdogo wa marudio.

Ametoa onyo hilo leo ambapo amesema kuwa wao kama CHADEMA wameamua kurudi kwenye uchaguzi licha ya ukweli kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) mpaka sasa hawajakiri kwamba kulikuwa na makosa makubwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 uliofanyika mwaka jana.

“Naionya Tume ya Uchaguzi (NEC) dhidi ya ukiukwaji, upuuzaji na uzalilishaji wa wapinzani kwenye uchaguzi. Ukiacha NEC, kimamntiki na kisheria wengine hawana mamlaka ya kusimamia uchaguzi kwa kuwa kuna chombo maalum chenye wajibu huo kisheria,”amesema Mbowe

Amesema kuwa Katika kata 26 mwaka jana waliwaona wakuu wa mikoa na wilaya wakisimamia uchaguzi, wakielekeza maofia wa NEC, na kuamuru udhalilishaji wa wagombea, mawakala na hata viongozi wa vyama vya upinzani.

Hata hivyo, ameongeza kuwa Maendeleo ya Demokrasia yamerudi nyuma kwa kiasi kikubwa, kwani wameamua kushiriki uchaguzi huo kwakuwa wamejiandaa kukabiliana na yeyote atakaye wanyanyasa.

t

Magazeti ya Tanzania leo Januari 23, 2018
Simba yaikung'uta Kagera Sugar