Mwenyekiti  wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na mbunge wa Hai, Freeman Mbowe  amesema tabia ya baadhi ya viongozi nchini, kuchochea ubaguzi wa kikabila ni hatari sana na kinapaswa kukemewa.

Amezungumza hayo wakati wa misa ya kumuaga Dk. Mengi leo tarehe 9 Mei 2019 katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Moshi mkoani Kilimanjaro, Mbowe amesema hayo kufuatia kauli za kibaguzi zilizotolewa na mtumishi mmoja wa serikali, ambaye jina lake hakuliweka wazi.

Amesema, “tuache kauli za kibaguzi. Tumuenzi Dk. Mengi, kwa vitendo. Mzee Mengi alikuwa mnyenyekevu na  alimpenda kila mmoja.

“Nashukuru Mhe. Ndugai uko hapa. Kazi ya Bunge ni kutetea maslahi ya wananchi. Teteeni maslahi ya wananchi mnaowawakilisha, kama kweli tunasema tumejifunza kutoka kwa Dk Mengi,” alisema askofu Dk Fredrick Shoo

Mbunge huyo wa Hai, mkoani Kilimanjaro eneo ambalo Dk. Mengi anatokea – alisema, “ukimuona mtu anatoa kauli za kudai kuwa kabila fulani halisaidii walemavu, ujue taifa linakwenda kubaya.”

Amesema, tabia ya kibaguzi zinapaswa kukomeshwa, hasa kwa taifa ambalo limejijengea heshima ya kuwa wamoja kwa muda mrefu.

“Tusitengane kwa makabila yetu. Naomba wale wote walioguswa na kauli ile, nitoe msamaha kwa kumuaga Mzee Mengi,” amesema Dk. Mengi na kuongeza;…..anapotokea kiongozi mwenye mamlaka wakatoa kauli za kibaguzi, lazima tuungane wote kupinga,” amesema Mbowe ambaye, alianza kwa kuomba radhi kwa kauli hiyo.

“Tuna nchi moja ambayo tunastahili kupendana, tunastahili kujengana, tunastahili kuheshimiana na tunastahili kumuona kila mmoja wetu ni sehemu halali ya nchi yetu.”

Amesema kuwa, hatua ya kuacha na kukubali kauli za kibaguzi, zitasababisha kupoteza utanzania wetu ambao ni moja ya sifa ya pekee.

Makonda aomba radhi kwa kauli yake kwa wachaga
Askofu Shoo awapa somo viongozi wa kisiasa

Comments

comments