Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amelaani kufungwa kwa Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Lindi, Selemani Methew, akisema kuwa kifungo hicho ni mkakati ulioandaliwa kudhoofisha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Kikao cha Kamati Kuu ya Chama hicho, Mbowe amewaagiza viongozi wa chama hicho nchi nzima kuandaa orodha ya kesi walizonazo ili waweze kuziwasilisha kwenye Jumuiya za Kimataifa ili kuonyesha upinzani unavyogandamizwa na kunyimwa haki.

“Selemani Methew alikuwa mgombea wetu wa Ubunge katika Jimbo la Mtama na wote mnafahamu kuwa tulishinda, amehukumiwa kwenda jela miezi minane, Mbunge wetu mwingine amehukumiwa miezi sita, huu mkakati uliopo wa kudhoofisha upinzani na kututisha ili tuache kufanya siasa,”amesema Mbowe.

Aidha, Mbowe ametaka kila kiongozi wa chama hicho aliye na kesi mahakamani afanye majumuisho  ili kuweza kufahamisha mahakama za haki za kibinadamu ili wajue jinsi upinzani unavyo kandamizwa nchini Tanzania.

Hata hivyo Mbowe amemkabidhi kadi ya uanachama aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini, David Kafulila kuwa mwanachama halali wa chama hicho.

 

Ummy Mwalimu anena kuhusu mafua ya ndege
Sheria ya makosa ya mitandaoni yaanza kung'ata