Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa vyama vya siasa nchini, Prof. Ibrahim Lipumba kuwa ni Profesa wa ajabu ambaye anaweza kubomoa misingi ya chama.

Ameyasema hayo wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani Mtwara, ambapo amesema kuwa hana ugomvi wowote na Prof. Lipumba ingawa amekiri kuwa atakuwa muongo akisema kuwa anamuheshimu kwani anatumika katika kukivuruga chama alichokuwa akikiongoza kwa muda mrefu.

Amesema kuwa wakati CUF ikishirikiana na UKAWA kutafuta kura na kuongeza idadi ya wabunge wa chama hicho bungeni, yeye Prof. Lipumba alikuwa mafichoni na anamshangaa sasa hivi anavyorudi ndani ya chama hicho na kutaka kukisambaratisha.

“Sina ugomvi na Prof. Lipumba lakini nikisema namuheshimu nitakuwa muongo sana. Prof Lipumba ni msomi sana tena msimchezee kwenye elimu lakini usomi ni jinsi unavyotumia elimu yako lakini siyo wingi wa vyeti. Ni Profesa wa ajabu kweli kweli. Mimi simuogopi mtu nitazungumza moja kwa moja,”amesema Mbowe

Hata hivyo, ameongeza kuwa kasi inayotumika kuibomoa CUF inatumika pia kuibomoa CHADEMA na kuweka wazi kuwa siku chama cha Chadema kikiuliwa labda awe amefariki lakini siyo wakati huu ambao bado anapumzi.

Serikali kupiga mnada ng'ombe 10,000
Kigwangala amshambulia Nyalandu, amkabidhisha kwa Takukuru