Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo, (Chadema), Freeman Mbowe amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kufikiria njia mbadala ya kuwaokoa watanzania dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona tofauti na zinazotumika sasa kwani madhara ya kiuchumi ni ya dunia nzima.

Mbowe ametoa ombi hilo kupitia ukurasa wake wa twitter, baada ya rais Magufuli kutoa taarifa kuwa tanzania haitafunga mipaka yake na wananchi hawataweka karantini kama nchi nyingine zilivyofanya kwasababu za kiuchumi na kutegemewa na nchi nyingine hasa kwenye matumizi ya bandari.

“Maisha ya watu hayawezi kurudishwa ila uchumi utatengenezwa, Rais Magufuli, Ulimwengu unalia na kuomboleza, uchumi wa dunia unaporomoka, uchumi wetu hauwezi ukatengamaa peke yake, Vifo vingapi vitakufanya uchukue hatua? Fanya lililo sahihi.” Ameandika Mbowe.

Jana wiazara ya afya ilitangaza vifo vya wagonjwa wawili wa Covid 19 wakazi wa Dar es salaam, Mmoja akiwa na umri wa miaka 51 na mwingine akiwa na miaka 57 na kufanya idadi ya waliofariki kwa ugonjwa huo hapa nchini kufikia watatu.

Halikadharika wizara pia ilitangaza waathirika wapya watano; wanaume wanne na Mwanamke mmoja. Wote ni wakazi wa Dar es Salaam. huku zanzibar ikitangaza kuongezeka kwa wagonjwa wawili , hivyo kwa sasa Tanzania bara na visiwani kuna waathirika wa virusi vya Coroana 32.

Billnass: Nampenda sana Nandy, nimechagua pande zote mbili
Mtihani mwingine A. Mashariki, Corona haijaisha Nzige wanarudi